Masisi : Hali imerudi shwari huko baada ya mituto ya risasi

Kimya imerudi tulivu tangu majuzi pa Nyabiondo ambako milio ya risasi ilimwangika kati ya jeshi la taifa FARDC na wanamugambo wa APCLS.

Duru zisizo za kijeshi zaeleza kwamba wanamugambo APCLS walikwenda kuvamia Ngome ya jeshi la taifa.

« Hapo hapo milio ya silaha kubwa na ndogo kujitokeza, ikidumu saa nyingi tangu saa kumi na moja za jioni hadi saa ine usiku, » aeleza mkaaji wa mahali.

Duru hizo zaongeza kwamba wanamugambo APCLS tayari wameacha senta ya Nyabiondo ili kuruhusu wakaazi kutoka nje na kwa watu wenyi kujeruhiwa kwenda hospitalini. Kwa hiyo watu kuanza tembea kwenyi barabara Nyabiondo Masisi.

Tufahamishe kwamba moto moja mwenyi umri wa miaka 5 kujeruhiwa na mwalimu moja wa shule la sekondari Nyabiondo kutekwa nyara hadi sasa.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire