Goma: Ajali ya barabarani ilisababisha vifo na majeraha

Commune de Goma

Watu sita kufariki dunia na wengine wengi kujeruhiwa. Matokeo ya ajali ya barabarani iliyojitokeza hii alhamisi tarehe 14

aprili 2022 kwenyi kata Mugunga mtàani Karisimbi mjini Goma.

Gari moja aina Fuso iligongana na jeep aina TX, mara moja Fuso kupinduka na watu sita kuaga dunia hapo hapo, na wengine wengi kujeruhiwa vikali.

 » Ilikuwa majira ya saa tano muda gari hizo kugongana na Fuso kupinduka watu sita waliokuwa ndani kufariki na wengine wengi kujeruhiwa. Tunaomba viongozi husika na kazi za barabarani kuchunguza swala hilo, » lanena shirika la raia la Mugunga.

Tufahamishe kwamba ajali za barabarani hufanyika mara kwa mara kwenyi barabara Mugunga Sake, zikisababishwa na mwendo wa kasi na hata ulevi wa madreva.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire