![](https://i0.wp.com/larondeinfo.com/wp-content/uploads/2022/04/img-20220415-wa00068309189297106739423.jpg?resize=678%2C305&ssl=1)
Raia wenyewe ni mashahidi kuona kwamba viongozi kadhaa wa kijeshi hawataki vita ikomeshwe mashariki mwa DRC walipo chukuwa madaraka. Tunaarisha kazi za zetu wakati mwengine, siyo kwamba tuna woga wakufungwa ama kuhamakiwa, ni namna ya kuepuka vuta ni kuvute kati ya raia na jeshi ama askari polisi ambao tunaunga mkono ili kufikia suluhu ya kudumu.
Matamshi hayo ni yake Jacques Sinzahaera mratibu wa Muungano wa mashirika hayo akisoma kikartasi mbele ya wandishi habari kwenyi jumba la UNPC mjini Goma.
Mashirika Amka Congo, Mouvement National Congolais pamoja na Congo conscience umekerwa kusikia kwenyi vyombo vya habari kwamba mea wa mji wa Goma azaniwa kufunga waandamanaji.
Pamoja na hiyo mwenyikiti wa mji wa Goma kutuma barua ya kukataza maandamano ,jambo ambalo halishangaze tena kwa kuwa hata viongozi wa kiraia walifanya hivyo wakikiuka katiba kwa kukataza maandamano ya Amani.
Barua hiyo iliyosomwa na Jacques Sinzahaera yaeleza kwamba kukataza wanamemba wa mashirika haya kuunga jeshi la taifa mkono ni kuunga mkono machafuko yote yenyi kufanyika mashariki mwa DRC.
« Kukataa tufanye kazi zetu za uraia ni moja wapo ya kukataza harakati za udemokrasia zitekelezwe nchini mwetu. Kukataa kuunga mkono jeshi letu la taifa, ni namna ya kuunga adui mkono ambaye anakwamisha usalama mashariki mwa nchi yetu » anena Jacques Sinzahaera akihitimisha kusoma kartasi mbele ya wandishi habari.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.