Nyiragongo : Watekaji nyara wa kijana mwenyi umri wa miaka ishirini walazimisha dola 1500 za marekani ili aachiliwe

Bosenibamwe Muzungu memba wa shirika la raia pa Nyiragongo.

Watekaji nyara walazimisha kiango cha pesa dola 1500 za marekani ili kijana wa umri wa miaka ishirini aachiliwe huru.Shirika la raia pa Nyiragongo laeleza kwamba kijana huyo alitekwa nyara juma tatu tarehe 11 aprili eneo la Muja kijiji Karungu na watu wenyi kumiliki silaha wasiojulikana.

 » Kijana kwa jina la Kalere alitekwa nyara siku nne sasa, akipatikana mikononi mwa wahalifu. Hawa wakilazimisha wapewe dola 1500 za marekani. Ijapo jamaa lake ni la wakulima, hawana chocote kile. Tunaomba serkali kujihusisha na swala hilo, ili kijana huyo aachiliwe  » anena Bosenibamwe Muzungu memba wa shirika la raia pa Nyiragongo.

Tufahamishe kwamba visa vya utekaji nyara eneo hilo la Kivu ya kaskazini ni chungu tele. Akina mama naye kwa jina la Kahindo Balemba aliye mja mzito alitekwa nyara, ni siku kumi sasa, akibaki mikononi mwa wanyanganyi , wakilazimisha dola elfu 3 za marekani kusudi aachiliwe.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire