Masisi: Muungano wa shirika la raia usultani wa Bashali laomba raia kuepuka habari za uongo zenyi kukwamisha usalama wakiarifu vyombo vya usalama

Shirika la raia la usultani wa Bashali laomba raia kwa jumla na hasa vijana kutoanguka katika mitego ya wafanya siasa, na kutopelekwa na kila upepo ili kuepuka usalama mdogo wa kudumu ndani ya wilaya ya Masisi.

Mwito ulitolewa hii ijumaa naye mratibu wa shirika la raia la usultani wa Bashali Justin Mpwiralwanda, kutokana na fununu za hapa na pâle ambazo ni moja wapo ya shida zinazoweza kwamisha maendeleo wilayani Masisi.

Shirika hilo la raia laomba watu kutofwata kila mtu, wakijiepusha na habari yoyote ile ya uchochezi na ya uongo, hasa kuarifu vyombo vya usalama.

Shirika la raia la usultani wa Bashali lapinga pia habari za uongo, kwamba waasi wa M23 wamejipenya wilayani Masisi. Na kuomba raia kuwa makini kwa kila habari yenyi lengo la kukwamisha usalama wilayani humo.

Tufahamishe kwamba habari hizo zimejitokeza kulingana na hali ya vita kati jeshi la taifa FARDC na waasi wa M23 wilayani Rutshuru.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire