Nyiragongo : Mtu moja kujiondolea maisha saa za alfadjiri

Mtu moja amejiondolea maisha asubui ya juma tatu tarehe 18 aprili 2022 ndani ya kijiji Kabaya Murongo usultani wa Munigi Kivu ya kaskazini.

Shirika la raia pa Nyiragongo laeleza kwamba ni majira ya saa kumi na mbili asubui ndipo Bwana kwa jina la Filire Luanda mwenyi umri wa miaka thelasini na mbili alijiuwa mwenyewe kwa kamba, wakati mkewe na watoto hawakukuwa nyumbani.

Duru zaeleza kwamba hayo yalisababishwa na hali mbovu ya maisha ya mhanga.

Tunalaumu kitendo hicho na kuomba raia kuwa na uvumilivu kwani mtu akikosa leo huenda kesho atapata, anena Bosenibamwe Muzungu memba wa shirika la raia la Nyiragongo.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire