Goma: Ayobangira Safari aomba wafanya siasa wa FCC warudi kwenyi meza ya mazungumzo kuhusu sheria ya uchaguzi

Mwanabunge wa taifa mchaguliwa wa Masisi Ayobangira Safari.

Mimi nawasii wanamemba wa muungano wa kisiasa FCC waingie kwenyi meza ya mazungumzo. Siyo vyepesi kufanya sheria ya uchaguzi yenyi kuridhisha watu wote. Tujaribu kotowa azimio zetu tukitaja shirika la raia, makanisa na hata sisi wabunge kila moja wetu atowe maoni yake. Mimi nitatowa ya kwangu. Baadae majadiliano yafanyike na uchaguzi kulingana na uwingi ulioko.

Hayo ni matamshi yake mwanabunge wa taifa mchaguliwa wa wilaya ya Masisi Ayobangira Safari, mbele ya wandishi habari kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma akitokea mji mkuu Kinshasa.

Mchaguliwa wa wilaya ya Masisi anena kwamba ni mhimu wenzake wa FCC wafahamu kwamba mazungumzo yatafanyika na pande husika, ila sheria ya uchaguzi itatekelezwa bungeni wakiweko.

Akisisitiza kwamba yeye ni moja wapo wa wanamemba wa muungano Union sacrée, na kuomba wenzake wa FCC wasipoteze muda kama ilivyokuwa mwaka 2015 tulipokataa operesheni ya oradha ya raia na kadhalika.

« Inabidi mbele ya yote tuwe na tume huru ya uchaguzi, tuwe na vikartasi vyote vya sheria ya uchaguzi, na twende kwenyi uchaguzi. Uwingi wa utawala utumike kwa manufaa ya nchi nzima bila kusahau hata upinzani« , anena Ayobangira Safari mchaguliwa wa Masisi.

Kuhusu mazungumzo kati ya waasi wa M23 na serkali, mwanabunge anena kwamba habari toka hapa na pale tayari zimemaanisha mazungumzo yenyewe. Akiomba serkali isije ikazungumze na kundi moja peke yaani waasi wa M23, bali na makundi zote zenyi kumiliki silaha, ambazo serkali iliahidi hiki ama kile ila hakuna kilichotekelezwa, na ndizo sababu za kudumu kwa vita.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire