Liwali wa jimbo la Kivu ya kaskazini Costant Ndima Kogba ametembelea wilayani Rutshuru majuzi ili kuwapa moyo askari jeshi kwenyi vita, pamoja na hayo kupongeza wenyi majeraha ya vita, na raia kwa jumla wilayani humo.
Duru zaeleza kwamba liwali mwanajeshi alikutana pia na makamanda wa operesheni na baadae kwenda kutembelea wahanga wa majeraha za vita wenyi kuwa hospitalini.
Baada ya hapo liwali wa jimbo la Kivu ya kaskazini alijielekeza pa Rwanguba barabara inayopelekea pa Bunagana ambako alikutana askari jeshi wakiwa uwanjani. Hawa walihakikisha kupigania nchi, wakitowa maisha yao yote.
Jenerali Constant Ndima aliwashukuru kwa bidii, kutokana na hatua walioichukuwa ya kutumikia taifa nzima.
Chumba cha wandishi
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.