Swala la usalama mashariki mwa DRC ilikuwa kiini cha kikao cha shauri kuhusu amani na usalama kilichofanyika kwa njia ya vidéo. Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ikiakilishwa naye waziri husika na mambo ya nje Christophe Lutundula.
Katika kikao, waziri huyo mkongomani aligusia hali ya usalama mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, kutekelezwa kwa makubaliano ya huko Addis Abeba na mpango wa kushiriki na kustawi mashariki mwa DRC
Washiriki kikao hicho cha Umoja wa Afrika walilaumu shambulizi kila leo ya waasi wa M23 mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, wakiomba waasi hawo kukomesha vita.
Shauri kuhusu amani na usalama la Umoja wa Afrika laahidi kuheshimisha hatua zilizochukuliwa na nchi mbali mbali.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.