Bukavu : Shirika nyipya la raia la Mulambula likiungana na mashirika mengine laomba barabara Bwindi hadi Kahero lifunguliwe

Waandamanaji waomba barabara lao lifunguliwe.

Katika tangazo lake la juma tano tarehe 20 aprili 2022, shirika nyipya la raia likiungana na shirika Maendeleo Kasha na muungano GIVODIM walikaa chini kwenyi kiingilio cha shule la sekondari Bwindi mtaani Bagira. Ni katika lengo la kulazimisha barabara Bwindi, Mulambula, Itudu hadi Kahero lifunguliwe.

Prezidenti wa shirika nyipya la raia tawi ndogo la Mulambula Awezae Cizungu Albert anayesahini tangazo anena kwamba imeandikwa kwenyi mabango yao: Shirika 5ème CELPA litupatie barabara yetu, hakuna maendeleo pasipo barabara, tunakataa kufungwa kwa barabara na viongozi wa shule la Bwindi na kadhalika.

Duru zaongeza kwamba waandamanaji walikaa chini tangu saa mbili hadi saa nne mbele ya mchana kati. Wakiahidi kwendesha viendo vikubwa hadi kufikia lengo

Upande wao, viongozi wa shule la Bwindi wahakikisha kwamba tayari waliweza pokea kibarua cha malalamiko cha wakaaji na hata kile cha kiongozi wa mtaa, ila hawana mamlaka, yote yatoka kwa Shirika lao 5ème CELPA.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire