DRC : Kila mfanya kazi wa serkali halali ataongezewa asilimia thelasini kwenyi mshahara yake mwishoni mwa mwezi aprili

Akihojiwa na wenzetu wa redio Okapi kuhusu kuongezeka kwa asilimia thelasini kwenyi mshahara ya kila mfanya kazi halali nchini DRC, waziri makamu wakwanza husika na mambo ya mambo ya wafanya kazi Jean Pierre Lihau anena kwamba ni uamzi wake raisi wa DRC Félix Antoine TSHISEKEDI ili kujibu kidogo kwa hali ya maisha ya wafanya kazi. Ijapo kuna mengi ya kutekeleza.

« Ni hatua yake raisi wa DRC ambaye alinena kwamba siyo wafanya kazi raia peke, hata askari jeshi na askari polisi wote wakiwa wafanya kazi wa serkali. Ni mwisho ya mwezi aprili ndipo wafanya kazi hawa wote wa serkali wataongezewa mishahara . Ni mhimu kukutana na waziri mkuu ili kuyazungumzia hata na washirika wetu kijamii pamoja na watumishi wa serkali wenyi kuwa kazini » anena waziri husika na feza.

Akihojiwa kuhusu malalamiko mengine ya wafanya kazi wa serkali, waziri anena kwamba yote yatajibiliwa moja kwa moja kwani vikartasi vya orotha ya watumishi wa serkali vyabidi kusahishwa.

Tutatowa shurti ili kusahisha vikartasi vya orotha ya watumishi wa serkali, Tunapashwa kufahamu kikweli orotha ya watumishi wa serkali, jambo halifahamike hadi sasa. Tunapashwa kuondowa vikartasi vyenyi majina peke« , aeleza waziri.

Waziri alifahamisha kwamba wafanya kazi 112 elfu ni tatizo kwa serkali akiongeza 300 elfu wazee ambao inabidi waache kazi, na kwamba shida hizo zinabidi suluhu ya pamoja. Kiongozi huyu wa serkali aonyesha kwamba pesa zitakazo ongezewa kwenyi mishahara ya wafanya kazi zatoka ndani ya mfuko wa serkali.

Huyu afahamisha kwamba inabidi kujuwa kwamba watumishi wa serkali wasaidia kuinua utajiri wa nchi na maendeleo, siyo tu kupokea pesa kama vile watu wengi huzani.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire