Goma: Shirika la kutetea haki za walimu wa shule za msinji SYNEEPP laundwa kulingana na makubaliano ya Mbwela Lodji ambayo wasema kutowafalia

Walimu wa shule la msinji lenyi kujumwika ndani ya shirika lenyi kuwatetea kwa jina la SYNEEPP wanajulisha kwamba tangu tarehe 2 mei 2022 wataanza mgomo kwa kuwa makubaliano ya Mbwela Lodji haikuheshimu haki yao. Wanaomba pia viongozi wa serkali kwa ngazi zote kutomshurtisha mwalimu aende shuleni bila kupata haki hake. Pamoja na hayo wazazi wacunge watoto nyumbani tangu tarehe 2 mei 2022.

Hayo yalikusudiwa katika mkutano mkuu wa walimu wa shule za msinji za serkali uliofanyika hii juma pili tarehe 24 aprili 2022 kwenyi shule la msinji Osso kato mjini Goma.

Walimu wa shule la msinji walichambua matokeo ya kikao cha Mbwela Lodji na kukusudia kwamba matokeo yenyewe yalifaulu kwa shule za sekondari peke wakiweka pembeni shule za msinji. Yafwatayo ni matamshi yake Sofia Valinandi mwakilishi wa walimu hii juma pili tarehe 24 aprili 2022 baada ya kikao.

Kulingana na mkutano wa walimu uliofanyika tarehe 24 aprili kwenyi shule la msinji Osso kato, walimu wa shule la msinji wenyi kujumwika ndani ya shirika SYNEEPP, wameona yafwatayo: Kwamba mkutano wa Mbwela Lodji haikuheshimu makubaliano yao ya kuwalipa walimu NU na NP trimestri ya kwanza ya mwaka. Hawakuheshimu makubaliano ya kulipa kiango ya pili na ya tatu ya mishahara ya tremestri hiyo hiyo. Hawakuheshimu kipengele cha pili cha makubaliano ya Mbwela, kwa kuwa pumzisha walimu ambao wamechoka ndani ya kazi. Hayo n’a mengineo hayakuheshimiwa anena Sofia Valinandi katika usomi wa tangazo kamili baada ya mkutano.

Shirika la kutetea haki ya walimu wa shule la msinji SYNEEPP lajulisha kwamba limeundwa kutokana na namna watetezi wao walioshiriki kwenyi mkutano wa Mbwela Lodji hawakujihusisha na madai yao, wakitetea haki zao binafsi na zile za walimu wa shule za sekondari.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire