Tommy Tambwe Mratibu husika na mpango wa huduma kwa walioweka silaha chini nchini DRC amejulisha kwamba ni muda wa kutekeleza mpango huo, kuanzia kwa kundi lililo kwenyi kempi ya Mubambiro.
Mpango huo wahusika na kupokonya silaha. kuondowa ndani ya makundi yenyi silaha na kuingizwa ndani ya maisha ya kawaida.
Mratibu husika na mpango huo kwa jina PDDRCS alinena hayo mbele ya wandishi habari mjini Goma, hii juma nne tarehe 26 aprili 2022. Pamoja n’a hayo atafwatiliya kazi hizo pa Kalunguta, Lubero na jimboni Kivu ya kusini, na kuunda kundi la mazungumzo husika na amani pia usalama.
Tunapenda kuhitimisha kwanza kazi hizo pa Mubambiro hadi kuwaingiza ndani ya maisha ya kawaida na kadhalika. Tutatumika haraka eneo za Kalunguta, Lubero na Kivu ya kusini maana mpango huo umekubaliwa asisitiza Mratibu husika na mpango wa huduma kwa walioweka silaha chini Tommy Tambwe.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.