Kivu ya kaskazini : Raia wahitaji amani ijapo uongozi wowote ule( Profesa Daktari Joseph Kitaganya)

Profesa Daktari Joseph Kitaganya azani kwamba ijapo uongozi wowote ule, wa kijeshi kama vile wa kirai jambo la mhimu ni kwamba raia wapate amani humu jimboni Kivu ya kaskazini.

Alinena hayo kwenyi vyombo vya habari vya mahali, kulingana na habari zenyi kusemeka hapa na pale kuhusu uongozi wa kijeshi humu jimboni Kivu ya kaskazini na hata huko Ituri.

Profesa Daktari Joseph Kitaganya asisitiza kwamba haegemee upande wowote ule, wa kijeshi kama vile wa kirai, ya mhimu ni kukomesha vitendo vya kinyama wanavyovitendewa raia kila leo yaani utekaji nyara, kukomesha kundi la wevi arubaini, mauaji na kadhalika, kwa kifupi ni kutekeleza amani.

 » Maoni yangu siyo kuwarudisha raia madarakani ama wanajeshi kuendelesha kazi ya uongozi wa Jimbo, kwangu binafsi natamani hali ya machafuko ikome, maana yake tuna haja ya amani, katika desturi yetu tuishi amani. Kwani pasipo amani hatuwezi tarajia maendeleo » anena mwana elimu huyo.

Akiongeza kwamba ahitaji aone kwenyi uongozi wa Jimbo mtu anayetumika sana kuhusu amani na usalama. Mtu ambaye anaweza komesha utekaji nyara, mauaji mjini Goma, kikundi cha wevi arubaini na kadhalika.

Akihojiwa mwishoe kuhusu mazungumzo kati ya serkali ya DRC na kundi zenyi kumiliki silaha inayofanyika mjini Nairobi, Joseph Kitaganya anena kwamba mazungumzo hayo ni mhimu, na siyo mhimu wakati haitowe suluhu kwa shida. Kwake mwalimu mkuu Joseph Kitaganya, mara kwa mara DRC huzungumza na makundi ya waasi bila suluhu kamili, na ingelibidi kubadili mbinu.

« Mimi nazani kwamba tuamshe zamiri karna hii ya 21. Tusitafute kutatuwa shida tukitumia nguvu, tuzungumze ana kwa ana, Tunakumbuka kwamba mazungumzo ya Sun city ilizaa 1+4, mazungumzo mengine na wanamugambo wa RCD, AFDL na kadhalika. Ingawa mazungumzo kisiasa na kidiplomasia haitowe suluhu sherti jeshi la taifa litumie nguvu na hii ni moja wapo wa jukumu la serkali ya DRC », ahitimisha matamshi yake Profesa Daktari Joseph Kitaganya.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire