Goma: Shirika lisilo la serkali husika na huduma kwa wanyonge IPEI laanzisha rasmi kazi mjini ili kupiganisha ukosefu kazi na umaskini

Shirika hilo IPEI kwa kifupi lilianzisha rasmi hii juma pili tarehe 30 aprili kazi likiweka mbele hizo za kutengeneza mikate. Yote yalifanyika katika ibada ili wanamemba wa Shirika na wengine waalikwa kumshukuru Mungu kwa kazi inayofanyika.

Pascal Mugisho mratibu wa Shirika IPEI kwa kifupi anena kwamba kazi hizo zalenga kuhudumia vijana na wanyonge mjini Goma na jimboni Kivu ya kaskazini.

« Tulipenda kuanza rasmi kazi zetu kupitia utengenezaji wa mikate. Tuliunda muungano wa wana vijiji kwa jina la AVEC ambao kwa sasa wanamemba ni 95. Kupitia mcango kidogo kidogo tunataka kukimbiza umaskini « aeleza Pascal Mugisho.

Huyu aomba viongozi wa serkali na mtu mwengine wa moyo mwema kuunga mkono kazi. Jambo ambalo aliunga mkono pia prezidenti makamu wa Muungano IPEI Bahati Birhashwirwa.

Mwalikwa maalum wa siku Pasta Moïse alinena ndani ya ibada kwamba inabidi kuweka Mungu mbele ili mradi huo ufaulu. Akiomba wanamemba kutumika bega kwa bega wakiwa na kauli moja.

« Wanamemba wa Muungano IPEI waungane, wazungumze kauli moja, wasigawanyike » akisisitiza mtumishi ambaye pia ni mwalimu wa yunivasti mjini Goma. Akiongeza yeye kuwa na ujuzi ndani ya sekta ya maendeleo ambayo huenda yatafalia kwa kazi za Muungano IPEI.

Bi Kavira Nicole moja wa waalikwa na mcuuzi wa mikate alishukuru kwa kazi hiyo ya kutengeneza mikate. Akiahidi kuhamasisha wenzake waje wengi kununua mikate ajili ya maendeleo ya Shirika.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire