Goma: Asilimia themanini na tano 85% ya walimu walianza mgomo wakibaki makwao

Asilimia themanini na tano ya walimu walianza mgomo hii juma nne tarehe 3 mei 2022 jimboni Kivu ya kaskazini. Wakijibu kwa mwito wa shirika la kutetea haki za walimu wa shule la msinji wakiomba serkali ya DRC kujibu kwa madai yao.

Mnenaji wa shirika hilo SYNEEPP kwa maarufu Sofia Valinandi anena kwamba kazi hiyo ilifaulu kwa kuwa walimu wengi walibaki nyumbani asilimia 85, na kama hakuna jibu mgomo utaendelea.

« Mgomo ulifaulu ipasavyo. Tunaomba serkali kujibu kwa madai yetu, kama sivyo mgomo utadumu hadi mwisho wa mwaka » aeleza mnenaji wa walimu.

Shule zimoja zilizo jaribu kufunguwa milango zilijikuta bila walimu, viongozi wa shule peke> pamoja na wanafunzi mfano wa shule la msinji Kesheni.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire