Nyumba saba zimetatizwa na kundi la wevi arubaini usiku juma tatu kuamkia juma nne tarehe 2 aprili 2022 kwenyi kitongoji Kasindi kata Katoyi mtaa wa Karisimbi Kivu ya kaskazini.
Habari toka vijana zaeleza kwamba wevi hao walipora vitu vingi ndani ya jamaa zilizo shambuliwa.
» Tuna huzuni kuona wizi huo kufanyika kando ya ofisi ya mtaa wa Karisimbi ambako idadi nyingi ya askari polisi yapatikana. Ijapo kelele ya raia hakuna msaada wowote ulionekana « duru toka vijana zaeleza.
Irafasha Cécile moja wa wahanga wa shambulizi hilo alaumu vitendo hivyo ,hasa ukosefu wa askari polisi wakati wa shida. Akiomba viongozi wa serkali kujihusisha kila mara na shida hiyo yenye kukumba wakaaji.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.