Akihojiwa na wandishi habari kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma Prezidenti wa pili makamu wa bunge la taifa Vital Banywesize Muhini anena kwamba ziara yake siyo ya kiserkali, ila akuja kupongeza wahanga wa mafuriko. Maji ya mto kusababisha vifo vya watu munane, nyumba nyingi kupelekwa na mengineo baada ya mvua kali ilionyesha.
« Ninafika Katika ziara isiyo ya kiserkali, ni yangu binafsi ili kuwapongeza wahanga wa mafuriko ya maji wilayani Kalehe, iliyosababisha vifo vya watu munane, nyumba kupelekwa na kadhalika » anena Prezidenti wa pili makamu wa bunge la taifa.
Vital Banywesize Muhini alisema kwamba ataunga mkono hatua ya liwali wa jimbo la Kivu ya kusini ambaye alikataza raia kujenga kila nafasi. Akihuzunishwa na maafa iliyojitokeza.
Prézidenti wa pili makamu alijibu kwa maswala mbali mbali akihakikisha kutekelezwa kwa uchaguzi mwaka 2023, swala la wanabunge wa taifa wasioshiriki kila mara kwa vikao lafwatiliwa kwa makini bungeni, swala kuhusu kuwa raia mkongomani ambalo halijapata kibali kwenyi bunge la taifa. Akisisitiza kwamba hakuje na msaada wowote ule ila hongera kwa ndugu zake wa Kalehe.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.