Kalehe: Mwili wa musichana usio na uhai umeogotwa

Wilaya ya Kalehe.

Mwili usio na uhai wa msichana mwenyi umri wa miaka kati ya 18 na 20 umekutwa alfadjiri ya ijumaa tarehe 6 mei pa Numbi eneo la Buzi wilayani Kalehe.

Mwili wa mhanga kwa jina la Anita Kalindula umekutwa kwenyi mto Nyabarongo kando ya kituo cha afya pa Numbi. Duru za mahali zaeleza kwamba msichana huyo alikuwa akifuwa mavazi mcana kati, ndipo watenda maovu kumucunguza.

Watenda maovu walimujeruhi vikali mbele auliwe na kumuacha hapo hapo. Na kwamba mhanga alikuwa mgonjwa wa kichwa, akiuliwa bila hatia yoyote ile.

« Tunaomba serkali kufanya ucunguzi ili kujuwa ni nani alitenda maovu hayo » anena mkaaji moja Bahati Rwamuhizi Jean Blaise.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire