Kivu ya kaskazini: Mwanabunge wa jimbo Alexy Bahunga afanya utetezi ili kuwatuma askari jeshi pa Mahanga kutekeleza usalama

Mwanabunge wa jimbo mcaguliwa wa wilaya ya Masisi anena hayo kutokana na hali ya heka heka majuzi, iliyo sababishwa na mapigano kati ya wanamugambo APCLS na wachungaji wenyi kushikilia silaha. Ni kwenyi umbali wa kilomita kumi na senta ya Nyabiondo.

Mwanabunge Alexy Bahunga mcaguliwa wa Masisi

« Ndani ya eneo la Mboko ya kwanza, kijiji Kasirosiro wachungaji wa mifugo waligongana na kundi mai mai lenyi kuleta hofu ndani ya eneo. Na hii yapelekea hofu ndani ya raia ambao zaidi ya miezi tatu waliishi ndani ya kimya. Raia watowa malalamika kusudi tuombe askari jeshi watumwe eneo hilo » anena Mubunge Alexis Bahunga.

« Akiongeza kwamba tangu askari jeshi waondoshwe, ngome za huko Mahanga zilibaki wazi. Tangu Mboko ya kwanza hakuna askari jeshi hata mmoja wa jeshi la taifa. Na hiyo yasababisha watu wenyi nia mbaya kuvuruga usalama eneo lenyewe, »anena mchaguliwa huyo.

Tufahamishe kwamba hali hiyo ya vita nikuvute kati ya kundi hizo mbili ilipelekea raia kuhama maskani yao, wakianza moja kwa moja kurudi sasa.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire