Kivu ya kaskazini: Muungano wa wavuvi wa ziwa Édouard unapiga kelele kuhusu njama za kuhamisha mpaka wa DRC

Ziwa Édouard.

Muungano wa wavuvi wa ziwa Édouard FECOPEIL unapiga debe kuhusu njama zenyi kutaka kuhamisha mpaka wa DRC kwenyi ziwa Édouard.

Katika kibarua kilichotumwa kwa liwali wa jimbo la Kivu ya kaskazini, muungano huo wanena kwamba hizo ni njama za vyombo vya usalama vya nchi ya Uganda.

Katibu tendaji wa muungano huo kwa jina la FECOPEIL anena kwamba hali hiyo yaharibu kazi za wavuvi kwenyi maji. uhusiano kati ya wavuvi na kati ya vyombo vya usalama vya nchi hizo mbili.

« Tunaarifu serkali ya DRC kupitia liwali mwana jeshi na serkali yote ya nchi kwamba nafasi upande wa DRC ni kilomita munane kwenyi ziwa Édouard. Kwa sasa mabadiliko yaonekana mpakani huko upande wa Kagezi hadi Chapa ndani ya DRC.Tangu kubadilishwa kwa mpaka huo, watu wa Uganda wameanza kuwafunga wavuvi wakongomani, hata kama kuna wavuvi wamoja wenyi kutambuka wakifwata samaki nchini Uganda. Tunaomba viongozi kufwatilia ili kutopoteza hata mita moja kwa DRC », anena katibu huyo tendaji.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire