Kivu ya kaskazini: Mwili wa mtu usio na uhai umegunduliwa mjini Butembo

Mji wa Butembo.

Mwili wa mtu usio na uhai umegunduliwa ijumaa tarehe 6 mei 2022 kitongoji Sabbat mtaani Bulengera mjini Butembo jimboni Kivu ya kaskazini.

Shirika la Bulengera laeleza kwamba mtu huyo alichomwa visu na watu wasio julikana, akirudi nyumbani kwake.

 » Usalama mdogo umepanda kiasi. Mara tena mwili wa mtu usio na uhai umekutwa mtaani Bulengera. Mhanga akiitwa kwa jina la Kapitula Thierry wa eneo la Kihyana, kata Kimbuli mtaani Bulengera mjini Butembo.

Tunaomba ucunguzi wa kweli ufanyike ili kujuwa ni nani aliyetenda maovu hayo, anena John Kameta présidenti wa shirika la raia la Bulengera. Akiomba viongozi kujihusisha na malalamiko ya raia . Shirika hili lasema kwamba laarifu kila mara viongozi na ni kwao kujihusisha. Likiangazia kwamba kwa ma saa ishirini na nne, watu wawili waliuliwa bila kufahamu msimamo wa viongozi wa serkali.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire