Kivu ya kaskazini : Mwanabunge jimboni Promesse aomba raia wapewe silaha ili kupambana na adui

Mwaka moja tangu utawala wa uongozi wa kijeshi Kivu ya kaskazini na Ituri, Mwanabunge Promesse Matofali asisitiza wapewe silaha raia ili kupambana na adui.

Akihojiwa na wandishi habari mjini Goma juma nne tarehe 10 mei, yeye afasiria kwamba ni njia moja wapo ya kukomesha usalama mdogo ndani ya majimbo hayo.

Promesse Matofali aonyesha kwamba utawala wa kijeshi haukufaulu inabidi ubadilishwe kwenyi madaraka.

Tangu kushimikwa kwa uongozi huo. tuliarifu kila leo kwamba hatuna jeshi lenyi kujiandaa vilivyo. Ndio maana tulionyesha kwamba shida yapatikana upande wa jeshi lisilo weza kupambana na vita yenyi kutatiza raia pa Beni. Hata kwenyi mjadala unaoandaliwa naye Raisi wa taifa, nitabaki kwenyi msimamo kwamba hakuna suluhu lingine, raia watolewe silaha., afasiria mcaguliwa huyo wa Butembo.

Akilinganisha na shambulizi dhidi ya Ukreno na Urusi, Promesse Matofali afasiria kwamba katiba na hata sheria ya nchi yamupa Raisi ruhusa ya kuwakabizi raia wamoja silaha, kukiwa sababu.

Tufahamishe kwamba mwaka moja tangu utawala wa kijeshi Kivu ya kaskazini, mnenaji wa kijeshi Jenerali Ekenge aangazia kuwa matokeo ni mhimu kwenyi uwanja wa mapambano kutokana na operesheni za pamoja Jeshi la taifa FARDC na UDPF ya Uganda.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire