Goma: Wana harakati Lucha Afrika waomba sekali Kivu ya kaskazini kupunguza malipo ya mtihani wa sekali

Muungano huo waomba serkali ya jimbo hususan liwali Costant Ndima kupunguza malipo ya mtihani kutokana na hali ya machafuko inayo kumba raia jimboni Kivu ya kaskazini kwa kiwango cha franka za kongo elfu 60 pahali pa elfu 121 kama alivyo amuru.

« Tuna kerwa kuona liwali wa jimbo aendelea kubaki kwenyi msimamo kutokana na kibarua alicho kisaini kwamba malipo ya mtihani wa sekali ni franka elfu 121 za kongo. Na hayo ni malalamiko ya raia walio wengi. Liwali wa jimbo hakupunguza malipo hayo, ijapo hali mbovu kiusalama na kiuchumi ambamo raia waichi, » anena Placide Itula memba wa wanaharakati wa Lucha Afrika.

Mwanamemba huyo aliendelea kutowa mfano wa Béni ambako raia wamekimbia maskani yao. Swala ni kwamba namna gani wanafunzi hao watatayarisha mtihani wakiwa ukimbizini, na namna gani wazazi ambao hawatumike watapata pesa ya kulipia watoto. Placide Itula aomba hawa wahudumiwe kipekee.

Shida siyo wilayani Béni peke, na hata Rutshuru ambako vita vyadumu, Masisi pia, na hata mjini Goma ambako raia waliteketea kutokana na mripuko wa volkeno na kadhalika.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire