Goma : Wakaaji toka soko ya Virunga hadi Katindo2 waomba aachiliwe huru dreva wao aliyepigwa na askari polisi bila hatia yoyote ile

Dreva moja mwenyi kutembeza barabara soko ya Virunga Katindo2 amejeruhiwa vikali kwa kupigwa kama nyoka na askari polisi hii juma tatu tarehe 16 mei 2022. Hayo yalifanyika wakati dreva alitaka kubeba wateja toka soko ya Virunga hadi Katindo2.

Akina mama moja miongoni mwa wateja tuliyemkuta eneo hilo anena kwamba anayo huzuni kuona dreva kupigwa na kupelekwa na askari polisi bila hatia yoyote ile.

Wachuuzi wenyi kutoka soko Virunga hadi Katindo2 waomba aachiliwe kijana aliyepelekwa na askari polisi bila kujuwa sababu. Wanaomba pia ucunguzi ufanyike na viongozi wa polisi katika lengo la kuazibu wana polisi wenyi kuzurura mjini, na wasio askari polisi wa barabarani.

Pamoja na hayo muungano wa madreva ACCO ufwatilie jambo hili maana miongoni mwa jukumu lake ni kutetea na kukinga madreva katika kazi zao za kila leo katika kuheshmu sheria ya uchukuzi.

Issa Lubiri.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire