Goma: Mtoto wa miaka tisa atekwa nyara pa Ndosho mtaani Karisimbi

Mji wa Goma.

Mtoto mwenyi umri wa miaka tisa alitekwa nyara hii juma pili tarehe 15 mei pa Ndosho, eneo Muabura mtaani Karisimbi.

Shauri la vijana pa Ndosho lanena kwamba mtoto kwa jina la Mikado alipelekwa na watu wasiojulikana. Wakilazimisha kiwango cha pesa asubui ya juma tatu kwa jamaa la mtoto ili aachiliwe.

« Wahalifu hawa walitupa kikartasi mbele ya mlango ya jamaa ya mhanga, wakishurtisha kiwango cha pesa. Tunalaumu vitendo hivyo haramu. Tunaomba viongozi kufwatilia na kukomesha hali hiyo » anena Claude Rugo prezidenti wa shauri la vijana pa Ndosho.

Tufahamishe tangu mwanzoni mwa mwaka 2022 zaidi ya visa kumi vya utekaji nyara vimeripotiwa pa Ndosho.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire