Goma: Shirika la kutetea haki ya walimu wa shule za msinji SYNEEPP latoa tahadhari kwa viongozi wa shule wenyi kulazimisha malipo kwa wazazi

Kikao cha walimu wa shule la msinji la serkali SYNEEPP.

Katika mkutano wa ucunguzi wa juma tatu tarehe 16 mei, shirika la kutetea haki ya walimu SYNEEPP maarufu latoa tahadhari kwa viongozi wa shule kadhaa za msinji za serkali ambao waomba malipo kwa wazazi ijapo shule za msinji za serkali ni bure.

Katika mkutano huo, shirika SYNEEPP laangazia kwamba kuna viongozi wa shule hizo za msinji wenyi kualika walimu kurudilia kazi, wakiahidi kuwalipa , na hiyo ni namna ya kuokowa mwaka wa shule. Shirika hilo laongeza kwamba serkali hayajibu madai ya walimu hadi sasa.

« Wakati huo walimu wamefurahi kuona mgomo uliheshimiwa nchini DRC hususan jimboni Kivu ya kaskazini. Ijapo viongozi wa shule za msinji za serkali wamoja waendelea kuomba malipo kwa wazazi na hiyo ni namna ya ukiukaji wa sheria iliyosainiwa naye raisi wa DRC kuhusu kusoma bure kwa shule za msinji, » laeleza shirika SYNEEPP wakati wa kikao kupitia msemaji Sophie Valinandi.

Shirika hilo laahidi kuzingatia mgomo hadi serkali itakapo jibu kwa madai ya walimu. tukitaja kulipa walimu wapya NU, kulipa kipande cha pili na cha tatu na mengineo.

Kupitia tangazo lilisomwa na msemaji wa SYNEEPP Sophie Valinandi, wazazi wabaki na watoto wao nyumbani hadi serkali atakapo jibu kwa madai ya wana elimu hawa.

Tufahamishe kwamba wilayani ya Masisi na ya Nyiragongo ziliwakilishwa kwenyi mkutano huo. Wakilishi wa wilaya hizi mbili waomba pia walimu wao kubaki nyumbani.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire