Masisi: Watekaji nyara walazimisha 1500 dola za marekani ili waachiliye mtoto

Masisi Kivu ya kaskazini.

Watekaji nyara wa mtoto Bahati Akilimali walazimisha dola 1500 za marekani ili aachiliwe. Huyu alitekwa nyara tangu tarehe 6 mei katani Birere pa Sake , eneo la Kamuronza.

Duru za mahali hunena kwamba watenda maovu hawo washurtisha wapewe mbele kiwango cha dola mia 300 za marekani za chakula kwenyi namba ya Airtel money.

« Tunaomba viongozi kujihusisha ili kuhitimisha hali hii jimboni Kivu ya kaskazini, hususan wilayani Masisi « shirika la raia la Kamuronza lanena.

Habari zaeleza kwamba jamaa la mhanga limekwisha tuma dola mia tatu za marekani zilizo shurtishwa ila mtoto hajaachiliwa huru,

Issa Lubiri.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire