Wanafunzi ishirini waliofaulu mtihani wamepokea tuzo toka Mwanabunge wa taifa Josué Mufula kupitia shirika lake, yaani bahasha, vitabu , kamusi na kadhalika.
Akiweko Prezidenti wa bunge jimboni Kivu ya kaskazini Robert Seninga, mwakilishi wa mea mjini Goma pamoja na viongozi wa shule nyingi miongoni mwao walimu wa lugha la kifransa walio rahisisha kazi za mtihani. Bila kusahau viongozi wafanyao kazi za utamaduni jimboni.
Sherehe hizo zililenga mtihani kielimu ajili ya amani mashariki mwa DRC, katika Mada: » wandishi ajili ya amani , DRC nyingine yawezekana »
Hayo yote kwa maandalizi ya shirika Josué Mufula kwa ushirikiano na shirika Mediaspol na washirika wengine.
Mwanabunge Josué Mufula alinena kujitowa ajili ya vijana , akikumbuka maisha ya kutumia silaha aliyoyaishi mbeleni angali bado mdogo. Akisisitiza kwa vijana kubadili mbinu, kuwapa vitabu vya shule na vinginevyo, na kwamba hiyo ni silaha kuhusu mabadiliko ya DRC.
« Ni namna ya kuonyesha kujitowa kwangu ajili ya vijana tangu miaka si nyingi. Ya mhimu kwa kipindi hiki cha pili, ni kutaka kuhitimisha mtihani tarehe 17 mei, siku ambayo ni historia maishani mwangu, nikikumbuka mengi. Nilikuwa mtoto mdogo, wakinipokeza silaha aina kalachnikov nifanye vita pahali pa kupigania amani. Kwangu siku hii, siyo ya kuwapa tena vijana silaha aina kalachnikov. Niwape vitabu ili waweze fikiri namna ya kubadili DRC. Twapashwa tia mkazo kwa vijana, kuwafunga utamaduni ajili ya amani, kuwapa fursa ya kujieleza kuhusu mada ya vita kutokana na vita vya kila leo jimboni na mjini », afasiria Mwanabunge Josué Mufula.
Mwanabunge huyu mtoto wa Goma aongeza kwamba ijapo vijembe shoka katika kazi za utamaduni jimboni Kivu ya kaskazini, atasonga mbele bila Shaka.
Upande wake Prezidenti wa bunge jimboni Kivu ya kaskazini Robert Seninga ashukuru shirika Josué Mufula na washirika wake kwa kutekeleza kazi kubwa. Akiahidi kuunga mkono kazi hizo kulingana na umuhimu wake. Jambo lililoungwa mkono na walio wengi walio shiriki kwenyi sherehe.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.