Masisi: Watu wafariki dunia kwa kupigwa risasi na jambazi

Watu wawili wamefariki dunia kwa kufyatuliwa risasi usiku wa juma tano kuamkia alhamisi tarehe 19 mei kwenyi senta ya Ngungu majira ya saa moja dakika hamsini usiku.

Duru za mahali zaeleza kwamba ni mwendesha pikipiki moja pamoja na mteja wake ambaye mfanya biashara , wakitokea Goma kuelekea Ngungu ndio walianguka ndani ya mtego. Hayo yalifanyika kwenyi shamba la Kasuku ambako watu hao walifariki, wajambazi kunyatuka.

Ni mwendesha pikipiki pamoja na mfanya biashara wakitokea Goma majira ya saa moja dakika hamsini ndio waliuliwa na jambazi wenyi kumiliki silaha. Mwendesha pikipiki kufariki hapo hapo na mfanya biashara akifariki ndani ya kituo cha afya cha mahali aeleza Hafashimana katibu wa shauri la vijana pa Ngungu ya kati.

Habari ilihakikishwa naye Ndagijimana Remera mjumbe wa liwali wa jimbo. Huyu aomba liwali kuongeza idadi ya askari jeshi pa Ngungu ya kati, kwani watu wauliwa kila leo mahali pale, Kazi ziliweza kuzorota kwa mda eneo hilo.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire