Goma: Mwili usio na uhai wa mwanamke umeonekana kutundikwa pa Kituku

Mji wa Goma.

Mwili wa akina mama mwenyi umri wa miaka sitini umekutwa ukitundikwa kwenyi mti juma tano tarehe 18 mei pa Kituku katani Kyesheo tukiwa mjini Goma.

Shauri la vijana laeleza kwamba mwili ulipatikana upande wa Kituku. Duru zaeleza kwamba yawezekana mhanga alinyongwa mbele auliwe .

Akili Norbert prezidenti wa shauri la vijana pa Kyeshero anena kwamba ni tangu asubui ndipo wakaaji walikuta mwili umetundikwa kwenyi mti. Ndipo kuharifu viongozi wa mahali.Kiongozi wa shauri la vijana aomba viongozi kulindia raia usalama, na kufanya ucunguzi ili kugunduwa watenda maovu hawo. Pamoja na hayo raia kujihusisha ndani ya kupiganisha usalama mdogo makwao.

Tufahamishe kwamba usalama mdogo ni kila leo pa Kyeshero , ambako yaripotiwa miili isiyo na uhai pamoja na visa vingine vya mauaji.

Juvénal Murhula.

.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire