Nyiragongo: Nyumba kadhaa zilibomolewa na mvua zilizonyesha

Eneo la Nyirragongo

Zaidi ya nyumba ishirini zilibomolewa pa Kibumba kutokana na mvua kali. Pamoja na hayo shamba kadhaa wilayani humo Nyiragongo juma nne tarehe 17 mei 2022.

Duru zaeleza kwamba hayo ni matokeo ya mvua kali ikisindikizwa na upepo mkali ndio ilisababisha maafa hayo.

Bosenibamwe Muzungu wa shirika anena kwamba vitu kadhaa vilipelekwa na maji ya mvua kutoka wakaaji.

« Tumehesabu nyumba ishirini, zaidi ya shamba thelasini kuharibika, vitu vya nyumbani havina hesabu, hata vifaa vya shule vya wanafunzi vilipelekwa na maji ya mvua, » anena Bosenibamwe Muzungu. Akiomba viongozi na watu wenyi moyo mwema kutoa msaada kwa wahanga. Kwa bahati, hakuna mtu aliyefariki dunia katika ajali hiyo.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire