Kivu ya kaskazini: Mwanabunge Patrick Munyomo atoa gari aina basi kwa muungano wake wa kisiasa AFDC ili kuwasaidia kikazi.Mwanabunge wa taifa Patrick Munyomo atoa hii ijumaa tarehe 21 mei gari aina basi kwa muungano wa kisiasa AFDC, wakati wa kusoma pia tangazo lililo hitimisha kikao, mda wa Siku mbili naye kamisa akitumwa n’a mkurugenzi wa chama Modeste Bahati Lukwebo.

Kikao kililenga kutafuta suluhu kwa mizozo iliyogawanya makada kadhaa wa chama hicho.

Msaada wake mwanabunge wa taifa Patrick Munyomo ulifurahisha wanamemba wa AFDC ambao waliahidi matumizi bora wakati wowote ule »: Basi hii itatusaidia sana kuboresha hali kijamii. Kuna wakati wa kulia n’a wakati wa kucheka, nazani gari hii itatusaidia sisi sote ndani ya chama. Mukipatwa na shida, fikeni mukajieleze, na Mungu awabariki » anena Kinyata Ruremesha Sylvestre kiongozi wa muungano wa chama AFDC jimboni Kivu ya kaskazini.

Upande wake mwanabunge Patrick Munyomo, kitendo hicho cha kukabizi wanamemba wa chama chake gari, ni namna ya kusaidia ili kutembea hapa na pale jimboni. Akiongeza kwamba hiyo ni alama ya kukumbuka wenzake wa chama jimboni Kivu ya kaskazini.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire