Kivu ya kaskazini: Kiongozi husika na maendeleo Remy Segihobe arudi mjini Goma toka mji mkuu Kinshasa ambako alifanya utetezi kuhusu usalama na maendeleo

Haitoshe kuongea kwenyi mitandao ya kijamii, kwenyi vyombo vya habari ama kuendelea kuteta viongozi ijapo hatuna uhakika kwa tunayo yatamka. Sisi tulipeleka mawazo na kupokelewa na washirika wa Raisi . Hawa waliahidi kufika na kujionea binafsi gisi hali ilivyo. Tuliomba watekeleze pendekezo zetu.

Haya ni matamshi yake Remy Segihobe mwanzilishi wa Redio Blessing FM, ambaye pia Kiongozi wa shirika linaloitwa kwa kina lake . Alinena hayo kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma hii juma pili tarehe 22 mei mbele ya wandishi, akiipokelewa na umati wa wanamemba wa shirika lake.

« Tunatoka mjini Kinshasa ambako tumepitisha wiki, tukitumwa na shirika lenyi kuitwa kwa jina letu. Ni shirika Rémy Segihobe ndilo liliandaa mradi kuhusu amani n’a maendeleo. Tuko mjini Goma. Hakuna asiyejua kama tunakumbwa na usalama mdogo. Tuliona umuhimu tukutanane na ngazi za juu, yaani Raisi wa nchi pahali pa kuendelea kuteta hapa na pale. Tulipokelewa kwenyi ngazi za Raisi na kutuacha tujieleze kuhusu usalama mdogo na maendeleo jimboni Kivu ya kaskazini, » anena Rémy Segihobe.

Akiongeza kwamba shirika Rémy Segihobe laendesha kazi sambamba akionyesha mfano wa umati uliofika kwa mapokezi kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma.

Remy Segihobe ambaye pia ni mwanzilishi wa Redio Blessing FM alinena kwamba mara kwa mara vibarua vyapelekwa mjini Kinshasa ila hakuna matokeo :Hata wanabunge wapita mara kwa mara kupeleka malalamiko ya raia, ila hakuna matokeo. Tulijiswali kuhusu malalamiko yetu, ingawa yamfikia Raisi wa nchi ama la. Na ndilo sababu ilitupeleka mjini Kinshasa alieza kiongozi hiyo.

Juvénal Murhula.Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire