Kivu ya kaskazini: Constant Ndima aalika vijana wa jimbo kuingia jesheni wakati wa kutoa ripoti ya semina kuhusu mwenendo na shurti kwenyi jeshi la taifa FARDC aliko shiriki mjini Kinshasa

Liwali wa Jimbo la Kivu ya kaskazini Jenerali Costant Ndima aomba vijana wasichana na wavulana wanaofaa kufanya kazi ya kijeshi, pahali pa kutuma waruga ruga kwenyi kazi hiyo.

Alinena hayo baada, ya kuhitimisha kikao ya kutoa ripoti kuhusu semina ya mafunzo ajili ya mwenendo na shurti kwenyi jeshi la taifa alimo shiriki mjini Kinshasa. Kikao ajili ya ma afisa wa ngazi zote jimboni Kivu ya kaskazini.

Mbele ya walikwa, liwali mwanajeshi anena kwamba ni matakwa yake Raisi wa DRC, kuhusu mabadiliko bora ndani ya jeshi la taifa,kutokana na shida zinazokumba sekta hiyo na kukwamisha maendeleo.

 » Semina ilifunguliwa rasmi naye Raisi wa DRC alhamisi tarehe 12 mei na kuhitimishwa juma mosi tarehe 14 mei 2022. Hakuna anayesahau mabaya yanayofanyika kila leo na viongozi wa serkali. Jambo limekwamisha maendeleo kijamii na kiuchumi nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Hali hii yaonekana pia upande wa jeshi. Na ni sababu moja wapo wa usalama mashariki mwa DRC na mengineo « alieleza Costant Ndima liwali mwanajeshi.

Upande wake msemaji wa serkali ya jimbo la Kivu ya kaskazini, Jenerali Ekenge akisoma kwa kiini yaliyozungumzwa ndani ya kikao mjini Kinshasa, akionyesha kwamba jukumu lahusu wote ili kuboresha sekta hiyo ya ulinzi. Kuanzia kwake Raisi wa DRC, bunge la taifa na seneti, serkali, ngazi za juu za kijeshi kila moja mahali alipo hadi kwenyi tabaka za chini.

Tufahamishe kwamba jambo kuhusu unyanyasaji ndani ya jeshi la taifa lilipelekea maswali mengi, ili kutafuta mbinu za kupiganisha hali kwa kuwa yawezekana.

Juvénal Murhula.


Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire