Kivu ya kaskazini: Jimmy Feruzi anena kwamba Prezidenti wa chama UNC Vital Kamerhe ataendesha kazi zake za kisiasa kwa kuwa ameachiliwa huru

Akiwasili kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma hii juma nne tarehe 24 mei, katibu mkuu makamu wa chama UNC chake Vital Kamerhe Jimmy Feruzi anena kuja jimboni akitumwa na katibu mkuu wa chama Billy Kambale ili kutumika na wanamemba jimboni. Kwa kutekeleza hiyo waita objectif 150 kwa kimombo. Akiongeza kwamba Prezidenti wa chama UNC Vital Kamerhe ameachiliwa huru na korti.

« Nawaletea ujumbe mhimu ambayo mwafahamu. Tangu jana tulipiganisha pamoja ili Prezidenti wetu apate uhuru. Nashukuru raia jimboni Kivu ya kaskazini, hususan wanamemba wa chama UNC na hata wa Muungano wa kisiasa Union sacrée, kwa kutuunga mkono. Mwafahamu kwamba Prezidenti wetu iko na jukumu hata kama yuko huru », anena katibu mkuu makamu Jimmy Feruzi.

Akiongeza kwamba hukumu aliyotolewa Prezidenti wa UNC toka korti tayari imevunjwa. Na kwamba atarudilia kazi zake kisiasa.

« Naamini Vital Kamerhe mtoto mashuhuri wa Kivu kwa jumla, atawasili mjini Goma siku za usoni, maana ni mji anayoipenda sana », aeleza Jimmy Feruzi.

Akiongeza kwamba anayo huzuni kutokana na raia wanaouliwa kupitia vita hapa na pale jimboni Kivu ya kaskazini, wamama wanaochinjwa na kadhalika. Jimmy Feruzi anena kwamba kazi nyingi zaandaliwa kwenyi uongozi wa chama UNC Kivu ya kaskazini yaani mafunzo kwa wanamemba, namna ya kuwatayarisha kwa kubuga ushindi kwenyi uchaguzi ujao na mengineo.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire