Kivu ya kaskazini: Ijapo milio ya risasi waziri wa kilimo nchini DRC Birihanze Nzinga aahidi kuendesha kazi ndani ya sekta yake

Waziri wa kilimo nchini DRC Birihanze Nzinga Desié.

Akiwasili kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma hii juma pili tarehe 30 mei 2022, waziri wa mambo ya kilimo Birihanze Nzinga Desié anena kuja ili kufanya kazi yake, ijapo vita vinavyokumba Jimbo la Kivu ya kaskazini.

.

Akishukuru juhudi za raia jimboni kwa kupinga mabeberu wanao kwamisha usalama humo, waziri aongeza kwamba serkali ya DRC inajitahidi ili kumgonga kila yule anaweza shambulia ardhi lake.

Ninashukuru raia jimboni waliosimama ili kupinga Wakaini kutovamia udongo wa DRC. Siyo siri Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo inajitahidi kumgonga kila yule ataweza kutaka kuvamia udongo wake. DRC haitashambulia mtu kwake, lakini kila atakayejaribu kushambulia maeneo yake atajionea cha mutema kuni. Nanena hayo kama mwana serkali, ahakikisha waziri mzaliwa wa Kivu ya kaskazini.

Waziri wa mambo ya kilimo Birihanze asisitiza kwamba atafanya kazi ijapo Hali ya vita inayokumba , na kwamba hakuna kitakacho zuwiya kutotenda.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire