Kivu ya kaskazini: Waziri husika na maendeleo vijijini na mwenziwe wa kilimo wapatikana ziarani jimboni Kivu ya kaskazini na kusini ajili ya kazi

Akiwasili kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma , waziri husika na maendeleo vijijini Francois Masumbuko Rubota anena kuja kwa niaba ya waziri mkuu Michel Sama Lukonde ili kufanya kazi.

« Nakuja jimboni Kivu ya kaskazini na kusini nikisindikizwa na mwenzetu wa kilimo ili kuhimiza raia kufanya kazi . Baadae kutengeneza barabara za vijijini ili kurahisisha mazao ya shamba kufika kwenyi miji mikuu » aeleza waziri mbele ya wandishi habari.

Akitumwa na waziri mkuu Michel Sama Lukonde, François Rubota Masumbuko amèna kwamba kazi hizo ni katika mpango wake Raisi wa DRC Felix Antoine Tshisekedi Tshilombo, ambaye ana lenga maendeleo kwa ngazi za chini.

Tukumbushe kwamba ni tangu miaka mingi, mimea kadhaa imekumbwa na ugonjwa kwenyi eneo zimoja jimboni Kivu ya kusini, mfano wa mumea wa mgomba kwenyi wilaya ya Walungu.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire