Bukavu : Kijana moja ajitundika ndani ya kanisa eneo la Route d »uvira

Mji wa Bukavu.

Kijana moja alikutwa amejitundika usiku wa juma nne kuamkia juma tano tarehe mosi juni 2022 ndani ya kanisa lake eneo la Route d »uvira, kata Ndendere, mtaani Ibanda.

Duru za mahali zanena kwamba huyu alikuwa mpiga nzenze yaani guitariste ndani ya kanisa yenyewe. Akizaniwa kutumiya kamba ya chombo hicho ili kujiondolea maisha.

Prezidenti wa shirika la raia mtaani Ibanda David Cikuru aeleza kwamba mhanga wa miaka takriban ishirini alikutwa kamba shingoni kwenyi mazabahu, na chanzo cha kujiuwa bado kujulikana.

Shirika la raia mtaani Ibanda lalaumu kisa hicho, likiongeza kwamba visa vya kujiuwa ni vingi siku hizi mtaani Ibanda, mjini Bukavu, jimboni Kivu ya kusini.

Issa Lubiri.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire