Goma : Nyumba zawaka moto kwenyi Kata Ndosho kitongoji 5 chantier

Mji wa Goma

Nimba kumi zimewaka moto kunako kitongoji 5 chantier kata Ndosho mtaani Karisimbi munamo usiku wa juma nne kuamkia juma tano tarehe 1 juni 2022. Prezidenti wa shauri la vijana kata Ndosho Marie Safi Macumo anena kwamba jamaa hizo zilipoteza vitu vya samani, na hazijue ziende wapi.

Huyu asema kwamba aliarifu shirika la kuzima moto ila hakuna kilicho fanyika. Akiomba viongozi wa serkali kujihusisha wakati wa shida aina hiyo.

Marie Safi aendelea kumbusha viongozi kutafuta suluhu ya zarura kuhusu jamaa hizi wahanga, kwa kuzitafutia makao, kutokana na usalama mdogo unaokumba hasa kata ya Ndosho. Kama sivyo jamaa hizo zitalala nje. Hadi sasa chanzo cha kuunguwa kwa nyumba bado kujulikana.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire