Kivu ya kusini: Miungano ya shirika la raia pamoja na wafanya siasa waomba DRC kukata uhusiano wowote ule na nchi ya Rwanda inayoshutumiwa katika shambulizi dhidi ya DRC

Waandamanaji mjini Bukavu.

Miungano ya shirika la raia pamoja na wafanya siasa waliandamana hii juma tano tarehe mosi juni mjini Bukavu, kwa kuunga mkono jeshi la taifa FARC kwenyi mapambano dhidi ya wagaidi wa M23 jimboni Kivu ya kaskazini.

Wakati wa màandamano wanamemba wa shirika la raia, wakijumwika ndani ya miungano Amka Congo, NDSCI, shirika la raia na vyama vya kisiasa walitamka rasmi kuunga mkono askari jeshi wa taifa, wakisema kijitowa hadi vita itakapokoma. kwenyi ardhi ya DRC

Katika kubarua walicho kutuma kwake Raisi wa DRC, hawa watoa pendekezo nyingi nakuomba serkali kuzitekeleza, ili kukomesha shambulizi kila leo ya kundi zenyi kumiliki silaha zikiungwa mkono na nchi ya Rwanda.

Pamoja waomba viongozi wa DRC kukata uhusiano kidiplomasia na Rwanda nchi yenyi kutajwa ndani ya shambulizi. Kufunga mipaka kwenyi ardhi, majini na hata hewani na nchi hiyo. Kupana malipizi kiuchumi kwa Rwanda na kusimamisha kazi za wafanya biashara kupitia mali wanayo nchini DRC. Kuvuta makubaliano yote iliyosainiwa kati ya DRC na Rwanda, hasa yenyi kuhusu uchimbaji madini ndani ya Kivu. Kukata ushirika wote kisiasa, kiuchumi, kiutu na hata kijeshi na Rwanda. Kuanza mashtaka kwenyi vyombo vya sheria vya kimataifa kuhusu machafuko waliyoitenda magaidi pamoja na washirika wao wakongomani, kubadilisha askari jeshi wa DRC waliotumika ndani ya kundi zenyi kumiliki silaha yaani RCD, CNDP na kadhalika na kuwatuma nafasi zingine za nchi, pia kuleta wengine wapya toka eneo zingine na mengineo.

Wakiomba Raisi binafsi kujihusisha ndani ya pendekezo hizo. « Tunakubali kupigana tukijitolea kuhusu DRC, ipate uhuru , umoja, na kuhusu raia waishimo . Tutaendelea kuunga mkono askari jeshi wetu katika operesheni zote za vita, ambao wapigania nchi na mipaka yake hadi kufikia ushindi,, » walitamka hayo walipokuwa wakiimba nyimbo kwa kuunga mkono jeshi la taifa FARC.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire