Muungano huo Lucha DRC AFRIKA mjini Goma waomba viongozi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kutangaza vita na nchi jirani ya Rwanda yenyi kuishambulia
Placide Itula moja wa wanaharakati hawo anena kuwa DRC, yalazimishwa kuomba vita na nchi ya Rwanda, kwani ni tangu miaka mingi nchi hiyo yashambulia DRC. Kabla ya hapo, serkali ichunguze kama inavyo vifaa vya vita. Pia kama hakuna ma beberu waliojipenya ndani ya jeshi la taïfa, kwa kuwa kila mara watu wenyi nia mbaya wajipenya ndani.
» Ni tangu miaka chungu télé nchi jirani ya Rwanda yashambulia DRC. Hatuwezi endelea kuvumilia hali hiyo, kwani raia ndio wahanga. Ma askari jeshi wa taïfa wamoja wajeruhiwa, wengine wapoteza maisha. Ni muda wa DRC, kutangaza rasmi vita na Rwanda. Ikijiandaa vizuri ili ya ushindi, »anena Placide Itula memba wa Muungano Lucha DRC AFRIKA.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.