Wahami wamoja waliokutana na wandishi habari wafahamisha kwamba warudi makwao kwani hawapate msaada na wamoja kati yao waanza kuchapwa makofi wakati wa kugawanya vitu.
« Mimi narudi kwangu ,tafazali kufia huko pahali pa kufia ndani ya Kempi, » anena Uwimwami Dorica mhami moja. Mwengine Hafashimwami Bahati asema kurudi ili kuendesha kazi zake za shamba. « Narudi pa Kibumba, mimi na jamaa langu kuendesha kazi za kilimo », aeleza.
« Mwendesha pikipiki wa Kibumba tuliyemkuta anèna kwamba Hali yaanza kuwa shwari huko.
Natokea pa Kibumba. Hakuna tatizo. Wakàazi wameanza rudi huko, ambako wapatikana pia askari jeshi wa taifa, » anena mwendesha pikipiki hiyo.
Tufahamishe kwamba wahami zaidi ya tano walijeruhiwa, wakipewa matibabu juma tano tarehe 1 juni , wakati wa kugawa vitu toka shirika PAM.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.