Nyiragongo: Mtu anayeshutumiwa wizi auliwa na raia Ngangi ya tatu

Kisa cha kujilipishia kisasi kimeripotiwa  ijumaa tarehe 10 juni 2022  kwenyi Kijiji Ngangi ya tatu majira ya saa kumi za asubui, kando ya nji wa Goma,  wilayani Nyiragongo Kivu ya kaskazini.

Prezidenti wa vijana Ngangi ya tatu anena ni kijana  waumri wa miaka ishirini n’a nne ndiye alinaswa akiiba televisheni.

 » Watu walimunasa n’a kumucoma ndani ya Kijiji Ngangi ya tatu, kando ya jumba Sainte Monique. Tunaomba raia kutojilipishia kisasi kwani wengi ni wahanga wasio n’a hatia », anena Prezidenti huyo wa vijana Ngangi ya tatu.

Kiongozi wa Kijiji hicho ahakikisha pia kitendo. Yeye alaumu kujilipishia kisasi kwa raia , akiwaomba kupeleka mshutumiwa mbele ya vyombo vya sheria. Na kwamba wengi hushutumia bila hatia. Kitendo hicho hakiruhusu serkali kufanya vema uchaguzi, kwani watenda maovu wengi hufichama moja kati yao anapouliwa , anena Kiongozi wa Kijiji Ngangi ya tatu.

Juvénal Murhula.

 

 

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire