Masisi : Watu saba kufariki dunia n’a wengine wengi kujeruhiwa na jambazi wenyi kumiliki silaha pa Kashuga

Watu saba miongoni mwao wanaume nne na akina mama tatu waliuliwa na wengine wengi kujeruhiwa na jambazi wenyi kumiliki silaha, pa Kashuga usultani wa Bashali Mokoto wilayani Masisi Kivu ya kaskazini.

Duru za mahali zaeleza kwamba jambazi hawo hawakujulikana, Ila jeshi la taïfa FARDC lilijitokeza bila kufaulu kuwa nasa.

Shambulizi lilifanyika usiku ndani ya Kempi moja ya wahami. Bahati Théophile moja wa viongozi wa mahali, alaumu kisa hicho mara tena, akiomba uchaguzi ufanyike ili kugunduwa watenda maovu hayo, na kuwapeleka mbele ya vyombo vya sheria, wakijibu kwa makosa yao.

Huyu aomba raia kutowa mapema wahalifu hawo, na kwa askari polisi kufanya kazi yao, Kwa kulinda raia na mali yao.

Tufahamishe kwamba shambulizi hilo lilifanyika baada ya shambulizi lingine lilijitokeza kunakuwa miezi kadhaa, na kusababisha vifo na majeraha.

Juvénal Murhula.

 

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire