Akihojiwa n’a wandishi habari kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma, Mratibu wa ligi ya vijana wa chama cha kisiasa ECD Éveil de la conscience pour le travail et le développement Bwana Fataki anena kuja mjini Goma ili kujioneya hali ya kazi za chama. Namna kazi za uongozi nyipya zilifanyika n’a mengineo.
Baada ya Goma, huyu atajielekeza jimboni Kivu ya kusini, Butembo n’a Béni, nafasi ambako chama kimeshimikwa.ijapo atatembea kote nchini DRC kuhusu lengo hilo.
Bwana Fataki anena Kwamba ECD memba wa muungano wa kisiasa FCC kinatumika sambamba mjini Kinshasa, ijapo wana siasa wengi miongoni mwao walikimbia muungano FCC.
Akihojiwa kuhusu vita vya M23 , Mratibu wa ligi ya vijana wa chama ECD asema kuunga mkono jeshi la taïfa FARDC, n’a kulaumu jeshi la kigeni kuvamia udongo wa DRC Kwa hiyo aongeza kwamba chama kinaendelea kufikiri kuhusu kuorozeshwa kwa vijana ndani ya jeshi, kama iliyo ombi ya walio wengi nchini DRC. Mratibu wa ligi ya vijana wa chama ECD nchini afahamisha pia kwamba chama chake kiko tayari kwenyi uchaguzi wa mwaka 2023, pasipo kutambusha hâta siku moja.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.