Kivu ya kaskazini/ Walikale: Jamaa nyingi hazina makao kwa sasa pa Mubi nyumba zao kuwaka moto

Habari toka pa Mubi wilayani Walikale zaeleza kwamba jamaa zaidi ya ishirini zalala nje ,nyumba zao zikichomwa kwa moto. Wahanga hunena kuteswa inje wakingojea msaada kutoka serkali, mashirika zisizo za kiserkali na watu wengine wa moyo mwema.

Sisi tunabaki nje bila makao, nikiwa na watoto tano.Tunakosa hâta vifaa vya ujenzi yaani mabati , mbao na kadhalika Tuna woga ya kulowana . Ndivyo tunaomba serkali kutujia n’a msaada maana tuna hatarisha maisha, anena mkaazi huyu wa Numbi tuliyemhoji kwa njia ya simu.

Mwengine husema kwamba moto ilijitokeza pasipo kujuwa, wakishituka kuona nyumba zao kuunguwa. Ila afahamisha kwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha ndani ya ajali. Naye aomba pia msaada kwa serkali n’a hâta kwa mashirika za kiutu, ili wapate namna ya kujenga n’a kuepuka kulala nje .

Upande wake mwakilishi wa liwali pa Numbi Kaputu Victor,


aomba viongozi wa jimbo kujihusisha n’a swala hilo. Akiomba kutuma vyombo vya kuzima moto eneo hilo, ambako mara na mara kunaripotiwa kuunguwa kwa nyumba.

Kutokana tu na duru zetu, ni mara ya nne kuunguwa kwa nyumba kwenyi senta Mubi munamo miaka tatu. Serkali ya jimbo na hâta île ya taïfa hazija fanyaka chochote kile kama msaada kwa wahanga.

Tufahamishe kwamba chanzo cha moto hakijajulikana hadi sasa. Raia walijaribu kuzima moto ila hawakufaulu.

Juvénal Murhula.

 


 


 

 

 

 

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire