
Mtu moja amefariki dunia akichomwa moto na raia wakimshutumu kuiba mbuzi. Hawa waliliipisha kisasi huko Bitongi juma mosi tarehe 2 julai 2022. Ni kwenyi kata Katambi eneo la Kanyabayonga, wilayani Rutshuru, Kivu ya kaskazini.
Duru zenyi kuaminika zanena kwamba mtu mwengine aliponea chupu chupu mikononi mwa vijana waliomfwata, akishutumiwa kosa hiyo.
« Tunalaumu watu hawa kuiba mbuzi ambayo tulikuta tayari imefariki. Hatuna haja ya wevi ndani ya eneo, » akionyesha hasira mkaaji moja wa huko ambaye hakupenda kutaja jina kwenyi vyombo vya habari.
Akihojiwa n’a wandishi habari wa Congoleo.net, kiongozi wa mahali Muhindo Lukira Pandasi ahakikisha habari. Huyu aomba vijana kutolipisha kisasi.
» Tuko na ofisi ya polisi, ofisi ya mahakama ya kijeshi n’a hâta ofisi ya mtaa. Ingawa tutaendelea kulipisha kisasi , tutafungwa na serkali, » akiarifu vijana.
Duru za mahali zaangazia kwamba visa vya kulipisha kisasi ni kila leo jimboni Kivu ya kaskazini, na kwa upeke pa Bitongi. Kiongozi wa mahali aongeza kwamba vijana wasahau kwamba ni serkali peke anayo mamlaka ya kuazibu.
Chumba cha wandishi.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.