Angola : Mkutano ana kwa ana Félix Antoine Tshisekedi n’a Paul Kaghame wafanana kutozaa matunda bora

Ni hii jumaa tano tarehe 6 julai ana kwa ana kati ya Raisi Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Paul Kaghame wa Rwanda huko Angola mbele ya mwenziwe wa nchi hiyo. Ana kwa ana ilihusu vita vya M23 wakiungwa mkono na nchi ya Rwanda dhidi ya jeshi la taïfa FARDC.

Duru zenyi kuaminika toka nchi ya Angola zaangazia gazeti la ronde info kwamba, hakuna kwa sasa dalili zinazo onyesha makubaliano kati ya Raisi hawo wawili.

Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, ashutumu nchi ya Rwanda kuunga mkono magaidi wa M23, ili kusababisha usalama mdogo, wakiendesha vita ambayo inasababisha vifo vya watu na wengine kukimbia maskani yao. Wakiishi katika hali ngumu uhamishoni.

Upande wa Rwanda, Paul amekanusha matamshi ya mwenziwe wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, kwamba nchi yake haiko nyuma ya waasi wa M23. Akishutumu pia serkali ya DRC, kuunga mkono waasi wa FDLR ,ili kushambulia nchi Rwanda.

Hadi sasa mazungumzo yaendelea, vita nayo yaendelea, kwa kungojea mjadala huo ufike ukingoni. Ni jambo la kufwatilia kwa makini.

Juvénal Murhula.

 

 

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire