Angola : Félix Antoine Tshisekedi na Paul Kaghame wakusudia kutafuta amani kuhusu vita kati waasi M23 n’a jeshi FARDC

Kushusha ugomvi ajili ya kurudisha hali ya matumaini kati ya Rwanda n’a DRC. Kushimikwa kwa mpango  wa kukomesha mapigano kati ya waasi wa M23 n’a jeshi la taïfa FARDC, na kuondoka kwa waasi kwenyi ngome wanazovamia nchini DRC.

Hayo ni miongoni mwa  pendekezo zilizochukuliwa baada ya mkutano ana kwa ana kati ya Raisi wa Rwanda Paul Kaghame pamoja naye Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo wa DRC pa Angola,  chini ya upatanishi wake Joâo Lorenço Raisi wa Angola. Uso kwa uso hii juma tano tarehe 6 julai 2022.

Raisi hawa wawili waligusia pia usawa wa uhusiano kidiplomasia kati ya nchi ya Rwanda n’a Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Tukumbushe kwamba tangu jana mwanzoni mwa majadiliano, ma Raisi hawa hawakuzungumza kauli moja. Wakati Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo alikuwa akishutumu Paul Kaghame kuunga mkono waasi wa M23 ili kuzorotesha usalama mashariki mwa DRC. Jambo lililotupiliwa mbali naye Paul Kaghame, akishutumu pia mwenziwe kuwa nyuma ya waasi FDLR, ili kushambulia nchi ya Rwanda.

Kwa wadadisi wa mambo, ni jambo la kuchunguza kwa makini.

Juvénal Murhula.

 

 

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire